Thursday, June 1, 2017

RONALDO AMFAGILIA MESSI.

MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amemsifu Lionel Messi na amesema anafurahia kumtizama akicheza nyota huyo wa Barcelona. Nyota hao wawili ndio wamekuwa wakitawala tuzo ya mchezo bora wa dunia kwa kipindi cha miaka tisa iliyopita na kila msimu wamekuwa wakifananishwa. Ronaldo ambaye kikosi chake cha Madrid kinatarajiwa kupambana na Juventus katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumamosi hii, amesema Messi ni miongoni mwa wachezaji ambao huvutiwa kuwatizama wakicheza. Ronaldo amesema huwa anafurahia kuwatizama wachezaji wote wazuri na Messi ni mmojawapo.

No comments:

Post a Comment