Thursday, June 1, 2017

MABAKI YA GARRINCHA YAIBWA.

Garrincha (kushoto) akiwa na Pele (kulia) enzi za uhai wake. 
FAMILIA ya nguli wa zamani wa soka wa Brazil, Garrincha imedai kuwa mabaki ya mpendwa wao yamepotea. Mabaki ya winga huyo ambaye alifariki dunia mwaka 1983 akiwa na umri wa miaka 49, yanadaiwa kuwa yanaweza kuwa yalipotea kwa kufukuliwa. Garrincha aliichezea Brazil mechi 50 kati ya mwaka 1955 mpaka 1966 na kulisaidia taifa hilo kutwaa Kombe la Dunia mwaka 1958 na 1962 wakati walipgawana kiatu cha dhahabu. Binti yake Rosangela Santos amesema baba yake hastahili hilo na ni jambo ambalo linakasirisha kutojua mabaki yake yalipo. Binti huyo aliendelea kudai kuwa meya alihidi kumtengenezea kaburi la kumbukumbu lakini wanahitajika kutafuta mabaki yake kwanza.

No comments:

Post a Comment