Thursday, June 1, 2017

TAIFA STARS YAENDELEA KUJIFUA MISRI.

KIKOSI cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kimewasili nchini Misri kwa ajili ya kambi yao ya mazoezi ya wiki moja. Mara baada ya kuwasili kikosi hicho kilipumzishwa kabla ya kuanza mazoezi jana usiku chini ya kocha wake Salum Mayanga. Akizungumza wakati wa mazoezi hayo jana usiku, Mayanga amesema walifanya mazoezi kwa saa mbili na wataendelea hivyo kwa kipindi chote watakachokuwa huko. Stars inajiwinda na mchezo wake wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika mwaka 2019 dhidi ya Lesotho ambao unatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Juni 10 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment