Thursday, June 1, 2017

MANCINI ATIMKIA ZENIT ST PETERSBURG.

KLABU ya Zenit St Petersburg imemteua meneja wa zamani wa Manchester City Roberto Mancini kuwa meneja wake mpya kwa mkataba wa miaka mitatu. Mancini mwenye umri wa miaka 52, mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa Italia, anachukua nafasi ya Mircea Lucescu ambaye alitimuliwa wiki iliyopita baada ya kuiongoza timu hiyo kwa msimu mmoja. Zenit walimaliza katika nafasi ya tatu katika msimo wa Ligi Kuu ya Urusi na kukosa nafasi ya kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Mancini alishinda taji la Ligi Kuu akiwa na City mwaka 2012, na hivi karibuni alitoka kuinoa Inter Milan. Meneja huyo raia wa Italia ambaye aliondoka Inter kwa makubaliano mwaka jana, anaweza kuongeza miaka miwili zaidi katika mkataba wake Zenit.


No comments:

Post a Comment