Friday, June 2, 2017

KEVIN DURANT AMFUNIKA LEBRONE JAMES WAKATI WARRIORS WAKIONGOZA FAINALI YA KWANZA YA NBA.

TIMU ya mpira wa kikapu ya Golden State Warriors imefanikiwa kuanza vyema mechi zake za fainali ya NBA kwa kuwachapa mabingwa watetezi Cleveland Cavaliers kwa vikapu 113-91. Nyota katika mchezo huo alikuwa Kevin Durant aliyeifungia Warriors alama 38 huku Stephen Curry akiongeza mitupo sita ya mbali yenye alama tatu kila mmoja. Mpaka robo mbili za kwanza zikimalizika, Warriors walikuwa mbele kwa vikapu 60-52 kabla ya kuendeleza kasi yao katika robo mbili za pili na kuibuka na ushindi huo. Warriors walitwaa taji la NBA mwaka 2015 kwa kuwafunga Cavaliers lakini walijikuta wakiteleza wakiwa na wanaongoza kwa 3-1 katika fainali za mwaka jana na kuwafanya Cavaliers kutwaa taji lao la kwanza. Timu hizo zinatarajiwa kukutana tena huko Oakland Jumapili hii katika fainali ya pili kati ya saba zitakazochezwa.

No comments:

Post a Comment