Friday, June 2, 2017

MONACO WAKATAA OFA YA ARSENAL KWA MBAPPE.

KLABU ya Arsenal, inadaiwa kukataliwa ofa yao ya paundi milioni 87 kwa ajili ya mshambuliaji wa Monaco Kylian Mbappe. Monaco inataka kumbakisha chipukizi huyo mwenye umri wa miaka 19 kufuatia pia kudaiwa kukataa ofa ya paundi milioni 105 kutoka Real Madrid. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na gazeti la Telegraph, kuna klabu nyingine ya tatu ambayo pia ofa yao imekataliwa. Klabu kadhaa kubwa Ulaya zimekuwa zikimfukuzia Mbappe zikiwemo Manchester United, Manchester City, Chelsea, Bayern Munich na Paris Saint-Germain-PSG.

No comments:

Post a Comment