Friday, June 2, 2017

GRIEZMANN ADAIWA KUFANYA MAWASILIANO NA MAN UNITED.

MSHAMBULIAJI nyota wa Atletico Madrid, Antoine Griezmann ameripotiwa kufanya mawasiliano na Manchester United baada ya rufani ya usajili wa klabu yake kutupiliwa mbali. Mahakama wa Michezo ya Kimataifa-CAS ilithibitisha kuwa adhabu ya kutosajili ya Atletico itaendelea kubaki kama ilivyo jana hivyo kumaanisha kuwa klabu hiyo iliyo chini ya Diego Simeone haitaweza kusajili mchezaji mpya mpaka Januari mwakani. Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa, anadaiwa kufanya mawasiliano na United na kuwahabalisha kuwa hataondoka Atletico kipindi hiki cha kiangazi. Atletico walikuwa wakiwafukuzia Alexandre Lacazette na Diego Costa ili kuchukua nafasi ya Griezmann mwenye umri w amiaka 26 msimu ujao, lakini sasa klabu hiyo haitaweza kupata mbadala wake hivyo kuamua kumbakisha.

No comments:

Post a Comment