Friday, June 2, 2017

LIVERPOOL KUIMARISHA OFA YAO KWA SALAH BAADA YA AWALI KUKATALIWA.

KLABU ya Liverpool, inadaiwa kuwa tayari kuimarisha ofa yao kwa Mohamed Salah baada ya ile ya paundi milioni 28 kukataliwa. Liverpool walitoa ofa hiyo baada ya kuzungumza na klabu ya AS Roma kuhusu nia yao ya kutaka kumsajili winga huyo wa zamani wa Chelsea lakini taarifa zinadai kuwa ofa hiyo ilikataliwa. Nyota huyo wa kimataifa wa Misri amekuwa akiwindwa na Liverpool ambao wanatafuta mchezaji mzuri anayweza kucheza pembeni katika kipindi hiki cha usjaili wa kiangazi. Meneja wa Liverpool anadaiwa kupewa kitita cha paundi milioni 150 kabla ya kwenda kucheza hatua ya mtoano kutafuta nafasi ya kutinga hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Salah ameifungia Roma mabao 19 akitokea pembeni msimu huu na kumfanya kuwaniwa na klabu kadhaa za Ulaya ambapo itaifanya Liverpool kutafuta walau paundi milioni 40 ili kunasa saini yake.

No comments:

Post a Comment