Friday, June 2, 2017

OZIL NJIANI KUSAINI MKATABA MPYA ARSENAL.

TAARIFA kutoka nchini Uingereza, zinadai kuwa kiungo wa Arsenal Mesut Ozil yuko tayari kusaini mkataba mpya na klabu hiyo. Taarifa hizo zinadai kuwa Ozil amekubali kupokea kitita cha paundi 280,000 kwa wiki badala ya paundi 350,000 kama ilivyokuwa ikidaiwa awali. Sababu kubwa za kuongeza mkataba mpya zinadaiwa ni kutokana na kutopata ofa yeyote makini kueleka kipindi hiki cha msimu wa mwisho wa mkataba wake. Mkataba mpya wa muda mrefu na kiungo huyo wa zamani wa Real Madrid inaweza kuwa mwanzo mzuri kwa Arsene Wenger ambaye naye amesaini mkataba wa miaka miwili.

No comments:

Post a Comment