Friday, June 2, 2017

BAADA YA GRIEZMANN KUPEPERUKA, MOURINHO AHAMIA KWA LACAZETTI.

MENEJA wa Manchester United, Jose Mourinho anadaiwa kujipanga kutenga kitita cha paundi milioni 50 kwa ajili ya mshambuliaji Alexandre Lacazette. Mourinho amehamisha nguvu zake kutoka kwa Antoine Griezmann aliyemtengea kitita cha paundi milioni 87 na kwenda mshambuliaji huyo wa Olympique Lyon kufuatia Atletico Madrid kufungiwa kusajili kiangazi hiki. Kushindwa kwa rufani ya Ateltico katika Mahakama ya Michezo ya Kimataifa-CAS, kumepelekea Atletico kuzuiwa kusajili kipindi hiki cha kiangazi hivyo kuondoa uwezekano wa kuweza kumruhusu Griezmann aondoke. Arsenal nao walikuwa wakimuhitaji Lacazetti lakini mwenyewe alikaririwa hivi karibuni akidai kuwa anataka timu inayoshiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa amefunga mabao 37 msimu huu, huku pia akifunga mabao 23 na 31 katika msimu miwili iliyopita.

No comments:

Post a Comment