Tuesday, June 6, 2017

ARSENAL YAFANYA USAJILI WAKE WA KWANZA.

KLABU ya Arsenal, imetangaza kuwa beki wa kushoto Sead Kolasinac anatarajia kujiunga nao kipindi hiki cha majira ya kiangazi akitokea Schalke 04 ya Ujerumani. Nyota huyo wa kimataifa wa Bosnia-Hrzegovina mwenye umri wa miaka 23, anatarajiwa kujiunga na Arsenal akiwa mchezaji huru na kuwa mchezaji wa kwanza kujiunga na timu hiyo pindi dirisha la usajili wa kiangazi litakapofunguliwa Julai mosi mwaka huu. Katika taarifa yake, Arsenal ilidai kuwa beki huyo anatarajia kuanza mazoezini kwa ajili ya msimu mpya mwezi ujao. Nao Schalke walithibitisha kuondoka kwa nyota wao huyo na kuongeza kuwa amepewa mkataba na Arsenal unaomalizika mwaka 2022.

No comments:

Post a Comment