Tuesday, June 6, 2017

PEPE ATHIBITISHA KUONDOKA MADRID.

BEKI wa kimataifa wa Ureno na Real Madrid, Pepe amethibitisha kuwa ataondoka katika klabu hiyo lakini amesisitiza bado hajakubali dili lolote na Paris Saint-Germain kufuatia kubainisha anaiwndwa na klabu za Uingereza. Pepe mwenye umri wa miaka 34, anamaliza mkataba wake mwishoni mwa mwezi huu na alikuwa akitaka kupewa mkataba wa miaka miwili Madrid. Lakini baada ya kupewa ofa ya mkataba wa mwaka mmoja, ameamua kuondoka kutoka katika klabu hiyo aliyojiunga nayo mwaka 2007 akitokea FC Porto. Akizungumza na wanahabari, Pepe amesema ni wazi hataendelea na Madrid na anakwenda kutafuta changamoto mpya.

No comments:

Post a Comment