Tuesday, June 6, 2017

SOUTHAMPTON YAIWEKEA KAUZIBE LIVERPOOL KWA VAN DIJK.

KLABU ya Southampton inatarajia kuishitaki Liverpool Ligi Kuu kufuatia tuhuma za kuwasiliana na beki wake wa kati Virgil van Dijkl kinyume cha utaratibu. Beki huyo mwneye umri wa miaka 25 ameshaweka wazi kuwa anataka kwenda Anfield kama akiondoka Southampton kipindi hiki cha kiangazi. Nyota huyo wa kimataifa wa Uholanzi anayekadiriwa kuwa na thamani ya paundi milioni 50, alisaini mkataba mpya wa miaka sita mwaka jana, kufuatia kujiunga na Southampton akitokea Celtic kwa kitita cha paundi milioni 13 mwaka 2015. Liverpool bado hawajaifuata rasmi Southampton na kuwaomba ruhusa ya kuzungumza na Van Dijk lakini kumekuwa na tetesi kuwa klabu hiyo tayari ilishamfuata na kufanya mazungumzo na mchezaji huyo.

No comments:

Post a Comment