Tuesday, June 6, 2017

WACHEZAJI WA MADRID KULIPWA ZAIDI YA BILIONI TANO KAMA BONASI.

WACHEZAJI wa Real Madrid wanatarajiwa kupewa bakshishi kubwa itakayovunja rekodi ili kuendana na msimu wa kihistoria waliopata. Madrid chini ya Zinedine Zidane aimefanikiwa kuwa klabu ya kwanza kufanikiwa kutetea taji lao la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuichapa Juventus mabao 4-1 katika hatua ya fainali Jumamosi iliyopita. Msimu wa 2016-2017 pia umeshuhudia Madrid wakitwaa taji la La Liga kwa mara ya kwanza toka mwaka 2012 na pia kufanikiwa kutwaa taji la Super Cup la Ulaya na Klabu Bingwa ya Dunia. Bakshishi kwenda kwa wachezaji kwa mafanikio hayo ya kutwaa mataji manne inadaiwa kufikia kiasi cha paundi milioni mbili kwa kila mchezaji. Msimu uliomalizika ndio wa kwanza baada ya kupita miaka 59 kwa Madrid kufanikiwa kutwaa mataji mawili kwa mpigo.

No comments:

Post a Comment