Tuesday, June 6, 2017

DORTMUND YAPORA KOCHA WA AJAX.

KLABU ya Borussia Dortmund imemteua meneja wa Ajax Amsterdam Peter Bosz kuwa meneja wao mpya kwa mkataba wa miaka 2019 kufuatia kuondoka kwa Thomas Tuchel. Bosz mwenye umri wa miaka 53 aliiongoza Ajax katika fainali ya Europa League mwezi uliopita ambapo walichapwa mabao 2-0 na Manchester United. Tuchel aliondoka Dortmund mwishoni mwa mwezi uliopita baada ya kuiongoza timu hiyo kwa miaka miwili. Tuchel aliiongoza Dortmund kutwaa taji la Kombe la Ujerumani msimu uliopita na pia kuwasaidia kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kushika nafasi ya tatu katika Bundesliga. Bosz alichukua nafasi ya Frank de Boer Ajax mwanzoni mwa msimu uliopita na alikuwa chini mkataba na klabu hiyo kutoka Amsterdam unaomalizika mwaka 2019.

No comments:

Post a Comment