Tuesday, June 6, 2017

LUKAKU KUONDOKA EVERTON.

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Ubelgiji, Romelu Lukaku amedai ni lazima aondoke Everton ili aweze kuimarika kama mchezaji. Lukaku amedai ameanza mazunyumzo na Everton kuhusu mustakabali wake na anataka kujiunga na klabu inayoshiriki michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na yenye uwezo wa kushinda taji hilo. Nyota huyo ambaye amefunga mabao 71 katika mechi 133 alizoichezea Everton, anawindwa na klabu za Chelsea na Manchester United na kusisitiza kuwa anataka kuhama ili kupiga hatua nyingine katika soka lake. Lukaku mwenye umri wa miaka 24 ambaye anathaminishwa kwa kitia cha paundi milioni 100 na Everton, amesema anafahamu anapotaka kwenda kwenda.

No comments:

Post a Comment