Wednesday, June 7, 2017

MAN UNITED YAIZIDI MADRID KWA UTAJIRI.

KLABU ya Manchester United imeipita Real Madrid katika orodha ya timu zenye thamani zaidi duniani kwa mujibu wa jarida la biashara la Forbes. United imetajwa kuwa thamani ya paundi bilioni 2.86 na kurejea kileleni kwa orodha hizo za mwaka kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka mitano. Klabu ya Barcelona ya Hispania inashikilia nafasi ya pili kwa kuwa na thamani ya paundi bilioni 2.82 wakifuatiwa na Madrid walioshuka mpaka nafasi ya tatu kwa kuwa na thamani ya paundi bilioni 2.77. Timu sita za Uingereza zipo katika orodha ya 10 bora, ambazo ni Manchester City, Arsenal, Chelsea, Liverpool na Tottenham Hotspurs. Mabingwa wa Ujerumani, Bayern Munich wako nafasi ya nne, wakati mabingwa wa Italia Juventus wako nafasi ya tisa. Madrid ambao wameshinda mataji ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na La Liga, wamekuwa wakiongoza orodha hizo kwa kipindi cha miaka minne iliyopita lakini wamekuta thamani yao ikishuka kwa asilimia mbili wakati United wao wakipanda kwa asilimia 11.

Forbes' top 20 most valuable football teams
1. Manchester United $3.69bn (£2.86bn)
2. Barcelona $3.64bn (£2.82bn)
3. Real Madrid $3.58bn (£2.77bn)
4. Bayern Munich $2.71bn (£2.1bn)
5. Manchester City $2.08bn (£1.61bn)
6. Arsenal $1.93bn (£1.5bn)
7. Chelsea $1.85bn (£1.43bn)
8. Liverpool $1.49bn (£1.15bn)
9. Juventus $1.26bn (£976m)
10. Tottenham $1.06bn (£821m)
11. Paris St-Germain $841m (£652m)
12. Borussia Dortmund $808m (£626m)
13. AC Milan $802m (£621m)
14. Atletico Madrid $732m (£567m)
15. West Ham $634m (£491m)
16. Schalke 04 $629m (£487m)
17. Roma $569m (£441m)
18. Inter Milan $537m (£416m)
19. Leicester City $413m (£320m)
20. Napoli $379m (£294m)

No comments:

Post a Comment