Wednesday, June 7, 2017

LIVERPOOL YATEGA KWA NYOTA WA SPORTING LISBON KAMA KIKISHINDWA KUELEWEKA KWA SALAH.

KLABU ya Liverpool iko katika mzungumzo na Sporting Lisbon kujaribu kumuwania mshambuliaji wao Gelson Martins kufuatia hofu ya kushindwa dau la winga wa AS Roma Mohamed Salah. Taarifa kutoka nchini Ureno zinadai Martins mwenye umri wa miaka 22, ameingia katika rada za Liverpool kufuatia mazungumzo na Salah kukwama baada ya ofa yao ya paundi milioni 28 kukataliwa. Roma wanaaminika kutaka kitita cha paundi milioni 40 ka ajili ya nyota huyo wa kimataifa wa Misri mwenye umri wa miaka 24, hivyo kuwaacha Liverpool kufikiria chaguo lingine mpaka hapo klabu hiyo ya Italia itakapokubali kushusha bei. Taarifa zinadai kuwa sasa Liverpool wameanza mazungumzo na Sporting Lisbon kwa ajili ya nyota huyo wa kimataifa wa Ureno ambaye ana kitenzi cha paundi milioni 50 katika mkataba wake.

No comments:

Post a Comment