Wednesday, June 7, 2017

MVUTANO WA KISIASA NCHI ZA GHUBA WALETA ATHARI KWENYE SOKA.

MVUTANO wa kisiasa kati ya Qatar na mataifa ya jirani ya ghuba, umepelekea mabadiliko ya viwanja vitakavyotumika kwa ajili ya mechi za Ligi ya Mabingwa barani Asia. Klabu za Persepolis ya Iran na Al Ahli ya Saudi Arabia jana zilipangwa kucheza mechi za robo fainali ya michuano hiyo za mikondo miwili. Mechi kati ya timu za Saudi Arabia na Iran tayari huwa zinachezwa katika viwanja huru kutokana na kuzorota kwa mahusiano ya kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili. Baadhi ya mechi zilichezwa katika mji mkuu wa Qatar, Doha msimu huu lakini sasa baadhi ya nchi za ghuba zimekata ushirkiano na Qatar. Jumapili hii, Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu-UAE, Bahrain, Misri na Yemen zilifunga ushirikiano na Qatar wakilituhumu taifa hilo kuunga mkono vikundi vye misimamo mikali.

No comments:

Post a Comment