Wednesday, June 7, 2017

MESSI AMTOSA LUIS ENRIQUE KWENYE HARUSI YAKE.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Argentina na klabu ya Barcelona, Lionel Messi anatarajiwa kufunga ndo na mpenzi wake wa siku nyingi Antonelle Roccuzzo mwishoni mwa mwezi huu. Katika harusi hiyo itakayofanyika nchini kwao Messi mwenye umri wa miaka 30 amealika wachezaji wenzake wote 21 kasoro meneja wake wa zamani Luis Enrique. Wawili hao wamekuwa wakiripotiwa kutokuwa na mahusiano mazuri na kulikuwa na taarifa kuwa ilikaribia kidogo Enrique atimuliwa katikati ya msimu wake wa kwanza kutokana na suala hilo. Nguli wa zamani wa Barcelona, Xavi pia aliamua kutomualika meneja yeyote wakati alipofunga ndoa yake na anatarajiwa kuwepo katika harusi ya Messi. Messi na Antonelle wamefanikiwa kupata watoto wawili wa kiume Thiago aliyezaliwa mwaka 2012 na Mateo mwaka 2015.

No comments:

Post a Comment