Wednesday, June 7, 2017

GIROUD AFIKIRIA KUONDOKA ARSENAL.

MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Olivier Giroud amekiri kuwa anaweza kufikiria kuondoka katika klabu hiyo kama hatapewa muda zaidi wa kucheza msimu ujao. Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa ameanza katika mechi 11 pekee msimu uliopita na kufanikiwa kufunga mabao 12. Wenger amekuwa akimpa nafasi zaidi nyota wa kimataifa wa Chile Alexis Sacchez badala ya Giroud. Sasa Giroud, ambaye alitoa pasi kwa bao la ushindi lililofungwa na Aaron Ramsey katika fainali ya Kombe la FA, anafikiri ni muda muafaka wa kuangalia mustakabali wake. Akizungumza na wanahabaro, Giroud amesema atazungumza na Wenger juu ya suala hilo na akiona hakuna ufumbuzi anaweza kufikiria kuondoka msimu ujao.

No comments:

Post a Comment