Wednesday, June 7, 2017

DORTMUND YANASA NYOTA KUTOKA FREIBURG.

KLABU ya Borussia Dortmund imemsajili kiungo wa kimataifa wa Ujerumani, Maximilian Philipp kutoka Freiburg kwa ada ya euro milioni 20. Dortmund ilitangaza usajili wa nyota huyo mwenye umri wa miaka 23 leo, baada ya kukubali mkataba wa miaka mitano. Philipp ameichezea Freiburg mechi 25 na kuisaidia kumaliza katika nafasi ya saba kwenye msimamo wa Bundesliga huku akifunga mabao tisa. Akizungumza na wanahabari, Philipp amesema Dortmund ni klabu kubwa duniani hivyo ni heshima kubwa kwake kuweza kuiwakilisha.

No comments:

Post a Comment