Wednesday, June 7, 2017

ALLEGRI ASAINI MKATABA MPYA JUVENTUS.

MENEJA Massimiliano Allegri amesaini mkataba mpya na Juventus ambao utamuweka kwa mabingwa hao wa Serie A mpaka 2020. Allegri aliisaidia Juventus kushinda mataji ya Serie A na Coppa Italia msimu huu huku akiowangoza kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Toka amechukua mikoba ya kuinoa klabu hiyo mwaka 2014 amekuwa akishinda taji la Serie A mfululizo. Allegri ambaye enzi zake alikuwa akicheza nafasi ya kiungo, alikuwa akihusishwa na tetesi za kwenda Arsenal kabla ya Arsene Wenger hajakubali kusaini mkataba mpya wa miaka miwili.

No comments:

Post a Comment