Thursday, June 8, 2017

MESSI AMMWAGIA MISIFA RONALDO.

MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Lionel Messi amesifu ubora wa Cristiano Ronaldo baada ya nyota huyo wa kimataifa wa Ureno kuisaidia Real Madrid kutetea taji la michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Messi na Ronaldo amekuwa akishindania tuzo mbalimbali duniani na Ronaldo kwa mwaka huu ndio anayepewa nafasi kubwa ya kutwaa Ballon d’Or. Akizungumza na wanahabaro kuhusiana na hilo, Messi amesema yeye na Ronaldo hawana uhasama wowote na kwamba jambo hilo limetengenezwa na vyombo vya habari. Messi aliongeza kuwa jambo kubwa kuhusu wao ni kila mmoja kutaka kufanya vizuri kila mwaka na kuzisaidia timu zao. Messi pia alidai siku zote amekuwa akitaka kumalizia soka lake Barcelona na ana matumaini hilo linawezekana kufuatia mazungumzo ya mkataba wake mpya kufikia pazuri.

No comments:

Post a Comment