Thursday, June 8, 2017

COSTA ATHIBITISHA KUONDOKA CHELSEA.

MSHAMBULIAJI wa Chelsea, Diego Costa amesema ameambiwa na meneja Antonio Conte kuwa hayupo katika mipango ya klabu hiyo. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 28 amefunga mabao 20 katika mechi 35 za Ligi Kuu na kuisaidia Chelsea kushinda taji lakini sasa anaonekana ataondoka Stamford Bridge. Akizungumza na wanahabari, Costa amesema bado yeye ni mchezaji wa Chelsea lakini hawamuhitaji tena kwani Conte ameshamwambia kupitia ujumbe mfupi kuwa hatakuwepo katika mipango yake msimu ujao. Costa aliongeza kuwa uhusiano wake na Conte haukuwa mzuri msimu huu, hivyo inabidi atafute changamoto nyingine. Costa ambaye ni mzaliwa wa Brazil mwenye uraia wa Hispania alijiunga na Chelsea akitokea Atletico Madrid kwa kitita cha paundi milioni 32 mwaka 2014.

No comments:

Post a Comment