Thursday, June 8, 2017

WARRIORS WABAKISHA MECHI MOJA WAWAVUE UBINGWA CAVALIERS.

TIMU ya mpira wa kikapu ya Golden State Warriors imepata ushindi katika mechi ya tatu mfululizo dhidi ya mabingwa watetezi Cleveland Cavaliers katika fainali za NBA zinazoendelea huko Marekani. Warriors walishinda kwa vikapu 118-113 na kuwafanya kuongoza kwa 3-0 kati ya mechi saba za fainali ya michuano hiyo. Kevin Durant alifunga alama 31 kwa Warriors na kuwafanya kubakisha ushindi katika mechi moja pekee. Kama wakifanikiwa kushinda mechi yao ya Ijumaa hii, Warriors itakuwa timu ya kwanza kutwaa taji hilo bila kufungwa mchezo hata mmoja katika fainali.

No comments:

Post a Comment