Thursday, June 8, 2017

CITY YAKAMILISHA USAJILI WA EDERSON.

KLABU ya Manchester City imemsajili kipa Ederson Moraes kwa kitita cha paundi milioni 35 kutoka Benfica ya Ureno. Kipa huyo mwenye umri wa miaka 23 aliibuka katika kikosi cha kwanza cha Benfica Machi mwaka jana ba kufanikiwa kuisaidia timu yake hiyo kushinda taji la Ligi Kuu ya Ureno na Kombe la Ligi. Akizungumza na wanahabari, Ederson ambaye atajiunga na City wakati dirisha la usajili litakapofunguliwa Julai mosi mwaka huu, amesema anapenda kila kitu kuhusu klabu hiyo. Ederson aliendelea kudai kuwa chini Pep Guardiola City inazidi kukua zaidi na zaidi na ni matumaini yake atasaidia kuleta mataji Etihad. Usajili wa Ederson unakuwa wa pili kwa Guardiola kipindi hiki cha majira ya kiangazi baada ya kumnasa kiungo Bernardo Silva kutoka Monaco kwa kitita cha paundi milioni 43.

No comments:

Post a Comment