Thursday, June 8, 2017

REAL MADRID YAITISHA UCHAGUZI.

MABINGWA wa Ulaya na Hispania, Real Madrid mapema leo wametangaza kuitishwa kwa uchaguzi wa rais wa klabu hiyo. Bodi ya uchaguzi ya klabu hiyo imetoa taarifa hiyo ambapo pia itashuhudia uchaguzi katika bodi ya wakurugenzi. Wagombea wanatakiwa kuwa wamejitokeza mpaka ifikapo Juni 18 na kama wakijitokeza mgombea zaidi ya mmoja bodi ya Uchaguzi itatangaza tarehe rasmi na mahali uchaguzi utakapofanyika. Rais wa sasa Florentino Perez aliiongoza klabu hiyo kuanzia mwaka 2000 mpaka 2006 na baadae kurejea kwa mara ya pili mwaka 2009 akichukua nafasi ya Ramon Calderon. Mwaka 2013 uliitishwa uchaguzi lakini Perez alikuwa mgombea pekee hivyo hakuna kura zilizopigwa. Madrid msimu huu wameshinda taji la La Liga ikiwa ni mara ya kwanza toka mwaka 2012 huku pia wakishinda taji la tatu la Ligi ya Mabingwa Ulaya katika kipindi cha miaka minne.

No comments:

Post a Comment