Thursday, June 8, 2017

RONALDO AONGOZA ORODHA YA WANAMICHEZO MATAJIRI.

MSHAMBULIAJI nyota wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo bado ameendelea kuongoza orodha ya wanamichezo 100 wanaolipwa zaidi, huku nyota wa Cleveland Cavaliers LeBron James akiwkwea nafasi ya pili kwenye orodha hiyo ilisheheni wachezaji wa NBA. Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ureno mwenye umri wa miaka 32, anakadiriwa kuingiza kiasi cha dola milioni 93, katika mshahara wake wa soka ambao ni dola milioni 58 na dola milioni 35 za mapato mengine ya matangazo. Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Ronaldo kuongoza orodha hiyo iliyotolewa jana, siku chache baada ya kuingoza Madrid kuifunga Juventus mabao 4-1 na kuwa timu ya kwanza kutetea taji la michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. James yeye anakadiriwa kuingiza kliasi cha dola milioni 86 na kumfanya kuwa mmoja kati ya wachezaji 32 wa NBA walioingia kwenye orodha hiyo. James anachukua nafasi ya Lionel Messi wa Argentina ambaye ameangukia katika nafasi ya tatu kwa kuingiza kiasi cha dola milioni 80.

No comments:

Post a Comment