Friday, June 9, 2017

SAGNOL AREJEA BAYERN KUMSAIDIA ANCELOTTI.

KLABU ya Bayern Munich imethibitisha beki wa zamani Willy Sagnol atarejea katika klabu hiyo kuwa msaidizi wa meneja Carlo Ancelotti. Sagnol ambaye amesaini mkataba wa miaka miwili, aliwahi kuichezea Bayern kwa kipindi cha miaka tisa na kufanikiwa kutwaa mataji matano ya Bundesliga na moja la Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2001. Shughuli za ukocha bado hazijawa na mafanikio makubwa sana kwake kufuatia kutimuliwa kuifundisha Bordeaux Machi mwaka jana. Sagnol anachukua nafasi ya Hermann Gerlan ambaye anakwenda kuendesha akademi ya Bayern kufuatia kuondoka kwa Paul Clement.

No comments:

Post a Comment