RAIS wa Shirikisho la Soka la Saudi Arabia, ameomba radhi baada ya kikosi cha timu yao ya taifa kukataa kusimama kwa dakika kwa ajili ya kutoa heshima kwa wahanga wa shambulio lililotokea darajani katika jiji la London. Wachezaji wa kikosi cha timu ya taifa ya Australia walishikana mikono kwa pamoja kama ishara ya heshima kabla ya mchezo wao wa kufuzu michuano ya Kombe la Dunia huko Adelaide Oval. Wakati wenzao wakifanya hivyo, wachezaji wa Saudi Arabia wao waliendelea kuchukua nafasi zao uwanjani huku wengine wakuonekana kunyoosha misuli yao. Tukio hilo lililaaniwa vikali na wasiasa akiwemo Waziri Mkuu wa Australia ambaye alilifananisha na ukosefu wa heshima. Hata hivyo, Shirikisho la Soka la Saudi Arabia, mapema liliomba radhi huku likijitetea kuwa kusimama kwa dakika moja ni nje ya utamaduni wao.
No comments:
Post a Comment