Friday, June 9, 2017

MOYES APIGWA FAINI.

MENEJA wa zamani wa Sunderland, David Moyes amepigwa faini ya paundi 30,000 baada ya kumwambia mwandishi wa BBC Vicki Sparks kuwa anaweza kupigwa makofi Machi mwaka huu. Kauli hiyo ya Moyes ilikuja kufuatia Sunderland kutoka sare nyumbani dhidi ya Burnley katika mchezo wa Ligi Kuu. Moyes aliulizwa na Sparks kama uwepo wa mmiliki wa Sunderland Ellis Short ulimuongezea shinikizo mpaka kupelekea kupata sare hiyo. Moyes ambaye alijiuzulu nafasi yake hiyo Mei, tayari alishaomba radhi kwa kauli hiyo aliyotoa dhidi ya Sparks.

No comments:

Post a Comment