Friday, June 9, 2017

ATLETICO YAJITOSA KWA COSTA PAMOJA NA KUFUNGIWA KUSAJILI.

KLABU ya Atletico Madrid inaripotiwa kufikiria kumsajili Diego Costa kipindi hiki cha majira ya kiangazi kabla ya kumpeleka kwa mkopo nchini China. Nyota huyo wa kimataifa wa Hispania anatarajiwa kuondoka Chelsea baada ya kuambiwa kuwa haitajiki na meneja Antonio Conte. Uamuzi wa Costa kuzungumza hadharani unamaanisha Chelsea inaweza kuamua kuamuacha mshambuliaji huyo kwa bei yeyote pamoja na kupoteza malengo yao. Costa mwenyewe anataka kurejea klabu yake ya zamani ya Atletico, baada ya kuondoka miaka mitatu iliyopita. Atletico wamefungiwa kusajili mpaka kipindi cha dirisha dogo la usajili Januari mwakani, hivyo wamepanga kumsajili Costa kasha kumpeleka kwa mkopo mpaka hapo atakapoweza kuitumikia klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment