Friday, June 9, 2017

JESUS AUMIA WAKATI ARGENTINA AIKIIFUNGA BRAZIL.

MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Gabriel Jesus amelazimika kutolewa nje kwa machela katika mchezo a kirafiki wa kimataifa kati ya Brazil na Argentina mapema leo baada ya kugongwa kichwani na mchezaji mwenzake wa City, Nicolas Otamendi. Otamendi alikuwa sehemu ya mabeki watatu waliopangwa na kocha Jorge Sampaoli katika kikosi cha Argentina ambacho kiliibuka ushindi mwembamba wa bao 1-0 kwenye mchezo huo. Wakiwa wanaongoza huku zikiwa zimeaki dakika chache mpira kumalizika, Otamendi alimgonga kwa kiwiko usoni mshambuliaji huyo wa Brazil wakati akijaribu kuokoa hatari langoni mwao na kupeleka Jesus kuanguka chini kabla ya kutolewa nje kwa machela. Kocha wa Brazil, Tite alidai mara baada ya mchezo huo kuwa Jesus alipata majeraha kidogo usoni na alikimbizwa hospitali kama tahadhari.

No comments:

Post a Comment