Friday, June 9, 2017

VERRATTI ANUKIA JUVENTUS.

WAKALA wa Marco Verratti amesisitiza kuwa kiungo huyo wa Paris Saint-Germain anataka kwenda klabu ya Juventus. Verratti mwenye umri wa miaka 24 ana mkataba na PSG unaomalizika mwaka 2021, lakini bado ameendelea kuhusishwa na tetesi za kuondoka klabuni hapo. Klabu kama Barcelona, Real Madrid na Juventus zimekuwa zikitajwa kumuwania nyota huyo wa kimataifa wa Italia katika miezi ya karibuni na sasa wakala wake Donato Di Campli amazidi kuchocheza moto kwenye tetesi hizo za kuondoka. Akizungumza na wanahabari, Di Campli amesema anategemea Juventus kufanya kitu muhimu katika usajili wa ujao. Di Campli aliendelea kudai kuwa PSG bado wanamuhitaji Verratti kwa gharama yeyote lakini mchezaji yeyote anahitaji kuwa katika timu ya ushindi.

No comments:

Post a Comment