Tuesday, June 13, 2017

GRIEZMANN ASAINI KANDARASI MPYA ATLETICO.

KLABU ya Atletico Madrid, Antoine Griezmann amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja na timu hiyo ambao unamalizika mwaka 2022. Mshambuliaji huyo nyota wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 26, amekuwa akihusishwa na tetesi za kwenda Manchester United, na mwezi uliopita alikaririwa akidai kuwa nafasi yake kwenda Old Trafford ni 6/10 kiangazi hiki. Lakini Griezmann alikubali kubakia Atletico baada ya klabu hiyo kufungiwa kusajili kipindi hiki cha kiangazi. Griezmann amesema jambo la kwanza anataka kuwaomba radhi watu kwa kutoelewa kauli yake aliyotoa. Griezmann aliendelea kudai kuwa toka ametua Atletico amekuwa akijituma kwa uwezo wake wote ili kuhakikisha wanapata mafanikio. Griezmann aliyecheza mechi 41 amefunga mabao 26 msimu uliopita na kuisaidia Atletico kumaliza nafasi ya tatu nyuma ya Barcelona na Real Madrid katika La Liga.

No comments:

Post a Comment