Tuesday, June 13, 2017

RONALDO ATUHUMIWA KUKWEPA KODI.

WAENDESHA mashitaka nchini Hispania wamemtuhumu mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo kwa kudanganya mamlaka na kukwepa kodi ya mamilioni ya euro. Ofisi ya mwendesha mashitaka jijini Madrid imesema imefungua kesi dhidi ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ureno. Waendesha mashitaka hao wanamtuhumu kwa kuwepa kodi inayokadiriwa kufikia euro milioni 14.7 kutoka mwaka 2011 mpaka 2014. Mara kadhaa Ronaldo alikaririwa akidai kuwa haofii chochote kuhusu uchunguzi wa kukwepa kodi anaofanyiwa kwnai hana lolote la kuficha.

No comments:

Post a Comment