Tuesday, June 13, 2017

EVERTON YAMNASA KIPA WA SUNDERLAND.

KLABU ya Everton, imekubali kumsajili kipa wa Sunderland Jordan Pickford kwa kitita cha paundi milioni 30. Pickford ambaye yuko katika majukumu ya kimataifa na kikosi cha Uingereza kwa vijana chini ya umri wa miaka 21, anategemewa kufanyiwa vipimo vya afya na masuala mengine muhimu pindi atakaporejea. Pickford mwenye umri wa miaka 23, anatarajiwa kuwa kipa ghali Uingereza kama akikamilisha usajili wake. Pickford aliichezea Sunderland mechi 29 za Ligi Kuu msimu uliopita lakini alishindwa kuzuia Sunderland isishuke daraja.

No comments:

Post a Comment