Tuesday, June 13, 2017

MORATA ANUKIA OLD TRAFFORD.

WAKALA wa Alvaro Morata amethibitisha kuwa mteja wake na Manchester United wanasubiri uamuzi wa Real Madrid wa kuamua kama watamuuza mshambuliaji huyo. United imekuwa ikihusishwa na tetesi za kumuwania nyota huyo wa kimataifa wa Hispania na kuna taarifa kuwa wlaikataliwa ofa yao ya euro milioni 60 wiki iliyopita huku Jose Mourinho akidaiwa kupanga kuongeza kutoa ofa mpya. Akizungumza na wanahabari, wakala huyo, Juanma Lopez amesema tayari kuna ofa kwa ajili ya mteja wake na wanachosubiri sasa ni uamuzi wa Madrid. Klabu ya AC Milan pia ilidaiwa kumuwania Morata ambapo Lopez amedai kuwa ofa yao ilikuwa ndogo na kuamua kwenda kumsajili mshambuliaji wa FC Porto Andre Silva. Morata amefanikiwa kuanza katika mechi 14 pekee La Liga msimu uliopita na Lopez amabeinisha kuwa mteja wake anataka timu atakayopata nafasi ya kucheza mara kwa mara.

No comments:

Post a Comment