Tuesday, June 13, 2017

IRAN YAWA YA PILI KUFUZU KOMBE LA DUNIA.

TIMU ya taifa ya Iran imekuwa ya pili kufuzu michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 kufuatia kuitandika Uzbekistan mabao 2-0 jijini Tehran. Mabao ya Sardar Azmoun na Mehdi Taremi yalitosha kuihakikishia nafasi hiyo Iran inayofundishwa na kocha Carlos Queiroz. Mabingwa mara tano wa Kombe la Dunia, Brazil ndio timu ya kwanza kufuzu michuano hiyo wakiungana na wenyeji Urusi. Timu mbili katika kila kundi kutoka bara la Asia zinafuzu moja kwa moja michuano hiyo huku zile zitakazoshika nafasi ya tatu zinakwenda kwenye hatua ya mtoano.

No comments:

Post a Comment