Tuesday, June 13, 2017

MILAN YANASA BEKI WA MEXICO.

KLABU ya AS Roma imetengaza kumsajili beki wa kimataifa wa Mexico Hector Moreno. Beki huyo mwenye umri wa miaka 29 anajiunga na Roma akitokea klabu ya PSV Eindhoven ya Uholanzi kwa ada ya euro milioni tano na kupewa mkataba wa miaka minne mpaka 2021. Moreno alikaririwa na tovuti ya klabu hiyo akieleza furaha yake ya kusajiliwa na Roma na kudai kuwa ni hatua muhimu katika maisha yake ya soka. Moreno ameitumikia PSV kwa misimu miwili sambamba na Mmexico mwenzake Andres Guardado na kusaidia kuipa taji timu hiyo msimu wao 2015-2016.

No comments:

Post a Comment