Wednesday, June 14, 2017

RATIBA LIGI KUU: MABINGWA CHELSEA KUANZA NA BURNLEY.

MABINGWA wa Uingereza, Chelsea wanatarajiwa kuanza kutetea taji lao nyumbani kwa kucheza na Burnley wakati msimu mpya wa Ligi Kuu utakapoanza mwishoni mwa wiki ya Agosti 12 na 13. Klabu zilizopanda daraja Newcastle United itaikaribisha Tottenham Hotspurs, wakati Brighton nayo ikiikaribisha Manchester City City na Huddersfield wao watakuwa wageni wa Crystal Palace. Mechi ya kwanza ya Spurs katika Uwanja wa Wembley watakaoutumia msimu ujao itakuwa ni dhidi ya Chelsea katika wiki ya pili ya msimu. Tarehe sahihi za mechi hizo zinatarajiwa kupangwa pindi ratiba ya luninga itakapoamuliwa. Ligi hiyo inatarajiwa kumalizika JUmapili Mei 13 mwaka 2018, ikiwa ni mapema zaidi kwa wiki moja ikilinganishwa na msimu uliopita kutokana na michuano ya Kombe la Dunia ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 14 nchini Urusi.

No comments:

Post a Comment