Wednesday, June 14, 2017

REAL MADRID YAMUUNGA MKONO RONALDO TUHUMA ZA KUKWEPA KODI.

KLABU ya Real Madrid imedai kumuunga mkono kwa asilimia 100 Cristiano Ronaldo baada ya mshambuliaji huyo kutuhumiwa kukwepa kodi na Mamlaka za Hispania. Mapema jana waendesha mashitaka wa Madrid walifungua kesi katika mahakama ya Pozuel de Alarcon wakimtuhumu Ronaldo kwa kukwepa kodi. Katika taarifa yao, Madrid wamedai kuwa toka Ronaldo atue katika klabu hiyo alionyesha ushirikiano wa wazi wa kufanya majukumu yake yote yahusuyo kodi hivyo klabu ina uhakika kuwa nyota wao huyo atakutwa hana hatia yeyote kwenye suala hilo. Tuhuma za Ronaldo zinakuja kufuatia nyota wa Barcelona Lionel Messi naye kuhukumiwa hivi karibuni kwa makosa kama hayo. Messi alikutwa na hatia mwaka jana na kuhukumiwa miezi 21 jela, lakini hataitumikia adhabu hiyo jela kwakuwa adhabu zote za chini ya miaka miwili mfungwa hupewa kifungo cha nje.

No comments:

Post a Comment