Thursday, June 15, 2017

BIRMINGHAM WAMTUPIA NDOANO JOHN TERRY.

MENEJA wa Birmingham, Harry Redknapp amedai kuwa klabu hiyo imetuma ofa ya mkataba kwa nahodha wa zamani wa kimataifa wa Uingereza na Chelsea, John Terry. Terry mwenye umri wa miaka 36 aliondoka Chelsea mwishoni mwa msimu uliopita baada ya kuichezea mechi 717 na kufanikiwa kushinda mataji 13 katika kipindi cha miaka 22.  Hata hivyo, Terry alifanikiwa kucheza mechi 14 pekee akiwa na Chelsea msimu uliopita. Akizungumza na wanahabari, Redknapp amesema wamemtengea Terry ofa nzuri na wamefanya kila wanaloweza hivyo ni juu ya mchezaji mwenyewe kuamua kuipokea au kuacha.

No comments:

Post a Comment