Wednesday, June 14, 2017

SUPER AGENT JORGE MENDES AITWA MAHAKAMANI.

WAKALA maarufu, Jorge Mendes ambaye miongoni mwa wachezaji anaowasimamia yupo Cristiano Ronaldo, ameitwa mahakamani nchini Hispania kufuatia tuhuma za ukwepaji kodi zinazomkabili mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia Radamel Falcao. Falcao anayecheza soka lake katika klabu ya Monaco hivi sasa, anatuhumiwa kushindwa kuweka wazi mapato yake ya euro milioni 5.6 zilizotokana na haki ya matumizi ya picha zake kati ya mwaka 2012 na 2013 wakati akiwa Atletico Madrid. Falcao anatuhumiwa kutumia kampuni za nje ikiwemo Visiwa vya Virgin, Ireland, Colombia na Panama ili kukwepa kodi. Mendes ameitwa kutoa ushahidi mahakamani Juni 27 mwaka huu jijini Madrid. Wito huo umekuja ikiwa imepita siku moja baada ya Ronaldo naye kutuhumiwa na Waendesha Mashitaka nchini Hispania kukwepa kodi ya euro milioni 14.7 kupitia kampuni za nje.

No comments:

Post a Comment