Monday, June 26, 2017

DONNARUMMA KUZUNGUMZA NA MILAN.

WAKALA wa kipa chipukizi Gianluigi Donnarumma, Mino Raiola amedai kuwa mteja wake huyo anatarajia kukutana na AC Milan ili kuweka mambo sawa baada ya michuano ya Ulaya kwa vijana chini ya miaka 21. Awali kipa huyo alieleza kuwa hatasaini mkataba mpya pindi mkataba wake wa sasa utakapomalizika mwakani, lakini mapema jana alituma ujumbe katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram akidai kuwa atatoa nafasi nyingine ya majadiliano ya mkataba mpya. Hata hivyo, kipa huyo mwenye umri wa miaka 18, ambaye ameripotiwa kuwindwa na klabu za Juventus, Real Madrid na Manchester United baadae alidai kuwa akaunti yake ya Instagram ilidukuliwa kabla ya kuifuta. Akifafanua mkanganyiko huo, Raiola amesema anakuwa akiwasiliana na Donnarumma kama marafiki na baada ya michuano ya Ulaya wanatarajia kukutana na Milan.

No comments:

Post a Comment