Monday, June 26, 2017

LYON YAKIRI ARSENAL KUMTAKA LACAZETTE.

RAIS wa klabu ya Olympique Lyon, Jean-Michel Aulas amesema Arsenal wako tayari kutoa fedha kwa ajili ya Alexandre Lacazette lakini yuko tayari kupambana kujaribu kumbakisha mshambuliaji huyo. Arsenal wamekuwa wakimtaka mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa kama mbadala wa Kylian Mbappe, kama meneja wa Arsene Wenger akishindwa kufanikiwa kumshawishi nyota huyo kutua Emirates. Wenger anaamini amefanikiwa kumshawishi Lacazette ambaye ameifungiwa Lyon mabao 37 msimu uliopita, kujiunga na Arsenal baada ya Atletico Madrid kukwama. Lacazette alikuwa ajiunge na klabu hiyo ya Hispania kipindi hiki cha majira ya kiangazi, lakini kufungiwa kusajili kulisitisha matumaini ya Atletico. Hata hivyo, Atletico wanadaiwa kuwa bado watamuwania nyota huyo Januari mwakani wakati adhabu ya kutosajili itakapomalizika.

No comments:

Post a Comment