Monday, June 26, 2017

MONACO YAMKOMALIA MBAPPE.

KLABU ya AS Monaco imeendelea kujipanga kuhakikisha wanafanikiwa kumbakisha Kylian Mbappe kwa mwaka mmoja zaidi. Mabingwa hao wa Ufaransa siku zote wamekuwa wakieleza nia yao ya kubaki na chipukiz huyo mwenye umri wa miaka 18 pamoja na kuwaindwa na klabu mbalimbali Ulaya. Mbappe anawania na klabu nyingi kubwa Ulaya baada ya kufanya vyema katika msimu wake wa kwanza katika kikosi cha kwanza cha Monaco ambapo amefunga mabao 26. Real Madrid wako tayari kumfanya chipukizi huyo kuwa nyota wao mpya wa Galactico, wakati meneja wa Arsenal, Arsene Wenger naye anataka kumpeleka Emirates kwa ahadi ya kumpa nafasi ya kucheza mara kwa mara. Monaco wamekuwa wagumu kidogo kumuachia Mbappe kutokana na kuondoka kwa nyota wao kadhaa mpaka sasa ambao ni Bernardo Silva aliyekwenda Manchester City, Tiemoue Bakayoko anayetarajiwa kwenda Chelsea, wakati Binjamin Mendy, Thomas Lemar, Fabinho na Djibril Sidibe nao pia wanaweza kuondoka.

No comments:

Post a Comment