Thursday, June 29, 2017

EVERTON YANASA BEKI WA BURNLEY.

KLABU ya Everton inakaribia kumsajili beki wa kimataifa wa Uingereza Michael Keane kutoka Burnley kwa kitita cha paundi milioni 25. Keane mwenye umri wa miaka 24 ameakuwa akiwindwa na meneja wa Everton Ronald Koeman na alishaweka wazi jinsi anavyomhusudu mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United msimu uliopita. Mazungumzo bado yanaendelea na Everton wana matumaini watakamilisha dili kabla wachezaji hawajarejea kwa ajili ya mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya Jumatatu ijayo. United nao walikuwa wakitajwa kutaka kumsajili tena Keane baada ya kuuzwa Burnley kwa kitita cha paundi milioni mbili na meneja wa wakati huo Louis van Gaal.

No comments:

Post a Comment