Tuesday, July 4, 2017

LEICESTER YANASA KIUNGO KUTOKA SEVILLA.

KLABU ya Leicester City imekubali kumsajili kiungo Vicente Iborra kutoka Sevilla. Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo ya Hispania imedai kuwa kila kitu kimeshakamilika na sasa kinachosubiriwa ni mchezaji huyo kufaulu vipimo vya afya. Iborra mwenye umri wa miaka 29, alihamia Sevilla akitokea Levante mwaka 2013 na kuisaidia kushinda mataji matatu mfululizo ya Europa League. Nyota huyo pia alicheza dhidi ya Leicester City katika mechi za mikondo miwili za Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita na kutolewa katika hatua ya motao ya 16 bora.

No comments:

Post a Comment